• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Wakenya 5 kuwania mataji ya kimataifa katika riadha

    (GMT+08:00) 2019-10-17 18:34:54
    Wakenya wanapigiwa upatu wa kutamalaki tuzo za Wanariadha Bora wa Mwaka duniani katika hafla itakayoandaliwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF) mnamo Novemba 23, 2019 jijini Monaco, Ufaransa. Wakenya Brigid Kosgei, Beatrice Chepkoech na Hellen Obiri wameorodheshwa kuwania taji la Mwanariadha Bora wa Mwaka kwa upande wa wanawake huku Eliud Kipchoge na Timothy Cheruiyot wakiunga orodha ya watimkaji watakaopigania tuzo hiyo kwa upande wa wanaume. Wanariadha wengine watakaopania kuwapiku Kipchoge na Cheruiyot ni bingwa wa dunia katika mbio za mita 800, Donavan Brazier wa Amerika, Mmarekani Christian Coleman ambaye ni bingwa wa dunia katika mbio za mita 100 na Joshua Cheptegei wa Uganda ambaue ni bingwa wa dunia katika mbio za nyika na mita 10,000.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako