• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yawahamisha watu kutoka sehemu zenye hali duni ili waondokane na umaskini

  (GMT+08:00) 2019-10-17 19:02:06

  Leo tarehe 17 Oktoba ni Siku ya Kupambana na Umaskini Duniani, na pia ni Siku ya kuondoa Umaskini ya China. Hadi sasa China imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa makazi kwa watu waliohamishwa kutoka sehemu zenye hali dunia ili waondokane na umaskini, na watu hao watapata makazi mapya kabla ya mwishoni mwa mwaka 2019.

  Katika kijiji cha Shuguangxincun cha tarafa ya Bojiaping wilaya ya Ningyan mkoani Hunan, familia 458 maskini zilizohamia hapa kutoka vijiji saba zimepewa nyumba nzuri mpya. Zamani waliishi katika vijiji vyenye hali dunia ya kiasili, na kukabiliwa na umaskini uliokithiri ambao ni vigumu kuondolewa. Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2017, walihamia kijiji cha Shuguangxincun. Katika kijiji hicho, vijana wakisaidiwa na serikali wamepata ajira. Feng Chunsheng anayefanya ufugaji wa kuku anasema,

  "Walinipa eneo hili, pamoja na mkopo na mafunzo husika, sasa nina uwezo wa kufuga kuku."

  Kuhamisha watu kutoka sehemu zenye hali duni ambazo ni vigumu kuondoa umaskini ni moja ya njia muhimu ya China kupambana na umaskini. Kwa mujibu wa mpango wa serikali kuu, China itahamisha watu maskini takriban milioni 10.

  Mkurugenzi wa idara ya ustawi wa mitaa ya Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Tong Zhangshun amesema, hivi sasa China imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa makazi kwa watu waliohamishwa kutoka sehemu zenye hali duni ili waondokane na umaskini, asilimia 96 ya makazi hayo yamekamilika, na zaidi ya watu milioni 8 wamepata nyumba mpya. Anasema,

  "Kazi ya kuwahamisha watu kutoka sehemu zenye hali dunia imeingia katika kipindi kipya. Asilimia 90 ya watu waliohamishwa wamepata misaada ya kupambana na umaskini, na takwimu zinaonesha kuwa kati yao zaidi ya watu milioni 7 wamefanikiwa kuondokana na umaskini."

  China inatarajia kumaliza kazi ya kuwahamisha watu wote kutoka sehemu zenye hali duni itakapofika mwishoni mwa mwaka huu. Hatua ijayo ni kuwasaidia kuondokana na umaskini kupitia ajira, elimu na afya. Naibu mkurugenzi wa idara ya kuhimiza ajira ya wizara ya nguvukazi na huduma za jamii ya China Bw. Yin Jiankun ameeleza kuwa, China itaongeza ajira kwa ajili ya watu maskini waliohamishwa, na kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi, akisema,

  "Tutawapatia watu wote waliohamishwa mafunzo ya ufundi stadi kwa kubainisha hali zao tofauti, na kuhakikisha tunawapa watu wenye nia na uwezo mafunzo kwa mara isiyopungua moja."

  China imepanga kuwasaidia watu wote vijijini kuondokana na umaskini uliokithiri kwa mujibu wa vigezo vya hivi sasa hadi mwishoni mwa mwaka 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako