• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya vifo vilivyotokana na mvua kubwa nchini Tanzania yafikia 29

  (GMT+08:00) 2019-10-17 19:18:52

  Polisi nchini Tanzania imesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania imefikia 29, wakati mamlaka ya hali ya hewa nchini humo ikitoa tahadhari ya kuendelea kwa mvua hizo.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Edward Bukombe ameliambia Shirika la Utangazaji nchini Tanzania (TBC) kuwa watu 18 walifariki katika mafuriko ya ghafla yaliyotokea katika wilaya za Korogwe, Handeni, Kilindi na Pangani yaliyosababishwa na mvua kubwa katika siku mbili zilizopita mkoani humo.

  Jumanne wiki hii, polisi walisema watu 11, wakiwemo wanafunzi watano, walifariki kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Morogoro.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako