• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais na waziri mkuu wa China wataka juhudi zifanyike kushinda vita dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:22:07

    Rais Xi Jinping wa China amezitaka idara mbalimbali kutekeleza malengo ipasavyo, kuendelea na juhudi za kupambana na umasikini uliokithiri, na kutatua matatizo yanayowakabili watu maskini katika elimu ya lazima, huduma za afya za kimsingi, nyumba na usalama wa maji, ili kuhakikisha watu maskini waishio vijijini wataondokana na umaskini na kuishi kwenye jamii yenya maisha bora.

    Rais Xi ametoa agizo hilo wakati China inapoadhimisha Siku ya 6 ya Kupambana na Umaskini hii leo. Rais amesema katika miaka 70 iliyopita tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, mafanikio makubwa yamepatikana katika vita dhidi ya umaskini, na tatizo la umaskini uliokithiri ambalo limesumbua taifa la China kwa miaka elfu kadhaa linatarajiwa kutatuliwa kihistoria, na huu utakuwa ni mchango mkubwa wa China kwa shughuli za kupunguza umaskini duniani.

    Naye waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametaka juhudi zifanywe ili kutimiza lengo lililowekwa la kuwawezesha watu wengine zaidi ya milioni 10 kuondokana na umaskini na kuweka msingi imara katika kushinda vita dhidi ya umaskini na kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako