• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Bei ya Unga wa Mahindi yatarajiwa kupanda

    (GMT+08:00) 2019-10-17 19:43:37
    Bei ya unga wa mahindi inatarajiwa kupanda tena baada ya wasagaji nafaka kumaliza magunia milioni 1.9 ya mahindi ambayo yalitolewa na serikali kwa bei nafuu Septemba 2019.

    Hali imeharibiwa zaidi na kupungua kwa uagizaji mahindi kutoka Uganda na Tanzania.

    Mmoja wa wasagaji nafaka mjini Eldoret,Bw David Kosgey,ameseme uhaba wa mahindi nchini pamoja na upungufu wa uagizaji kutoka Uganda na Tanzania umefanya bei ya mahindi kupanda.

    Aidha alisema hawana budi ila kupandisha bei ya unga.

    Kiwango cha mahindi kinachoingizwa kutoka Uganda kimepungua katika muda wa miezi miwili iliyopita na kufanya gunia la kilo 90 kuuzwa kwa Sh3,200 kutoka Sh2,800.

    Mahindi kutoka Tanzania yanauzwa kwa Sh3,400 kutoka Sh3,000 kwa kila gunia la kilo 90.

    Kulingana na Baraza la Nafaka Afrika Mashariki (EAGC), uhaba wa mvua unaweza kufanya mavuno ya mahindi kupungua Uganda, Tanzania na Kenya na hivyo basi kusababisha bei ya unga kupanda zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako