• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China kuisaidia Afrika kutimiza ajenda ya mageuzi

  (GMT+08:00) 2019-10-18 08:56:20

  Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lililotolewa na China limetajwa kuwa linaweza kuchukua nafasi muhimu katika kuisaidia Afrika kutimiza ajenda yake ya mageuzi ya kiuchumi.

  Mwenyekiti wa Sekritarieti ya Kenya ya Utaratibu wa Kufanyiana Tathmini wa Afrika katika Baraza la Usimamizi wa Kitaifa wa Ushirikiano Mpya kwa Maendeleo ya Afrika Bw. Michael Chege, amesema mjini Nairobi kuwa kuna mambo mengi yanayofanana kati ya pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Ajenda 2063 ya maendeleo ya Afrika.

  Akiongea kwenye mkutano kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika ulioandaliwa na chuo kikuu cha Nairobi, Bw. Chege amesema pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja linaisaidia maendeleo ya miundombinu barani Afrika, ambayo utafiti umeonesha kuwa asilimia 25 ya maendeleo ya miundombinu katika miaka 18 iliyopita yamegharamiwa na serikali ya China, huku serikali za nchi Afrika zikigharimia asilimia 40.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako