• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wapitisha makubaliano mapya kuhusu Uingereza kujitoa umoja huo

  (GMT+08:00) 2019-10-18 09:17:58

  Viongozi wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya isipokuwa Uingereza jana wamefikia makubaliano na kupitisha azimio la kuunga mkono makubaliano mapya yaliyofikiwa kati ya kamati ya umoja huo na serikali ya Uingereza.

  Viongozi wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya jana alasiri walianza mkutano wa siku mbili huko Brussels, ambapo viongozi wa nchi 27 isipokuwa Uingereza wamepitisha azimio hilo. Azimio hilo pia limezitaka kamati ya Umoja wa Ulaya, bunge la Ulaya na bodi ya Umoja wa Ulaya zichukue hatua za lazima ili kuhakikisha makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa rasmi tarehe 1 Novemba.

  Baada ya mazungumzo magumu, kamati ya Umoja wa Ulaya jana asubuhi ilifikia makubaliano mapya na serikali ya Uingereza. Baada ya kukubaliwa na viongozi wa nchi 27, makubaliano hayo bado yanahitaji kupitishwa na bunge la Ulaya na bunge la Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako