• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yasema itapunguza utekelezaji wa ahadi kuhusu nyuklia kama pande mbalimbali zitashindwa kulinda maslahi

    (GMT+08:00) 2019-10-18 09:37:07

    Iran imesema itapunguza zaidi ahadi zake kama pande zilizosalia katika makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA zitashindwa kuisaidia nchi hiyo kupata manufaa ya kiuchumi kupitia makubaliano hayo.

    Mkuu wa wafanyakazi wa ofisi ya rais wa Iran Bw. Mahmoud Vaezi amezungumzia kile alichokiita kuwa Umoja wa Ulaya kutotekeleza wajibu wake chini ya makubaliano ya nyuklia, akisema kama Ulaya haitatekeleza ahadi zake, basi Iran itachukua hatua zaidi.

    Tangu mwezi wa Mei Iran imechukua hatua tatu ikiwemo kujenga ghala ya fueli ya nyuklia na kurutubisha madini ya uranium. Pia imeanzisha vifaa vya kurutubisha uranium ili kuongeza akiba yake ya uranium iliyorutubishwa, hatua inayopigwa marufuku kwenye makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako