• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: KPL sasa yasema 'serikali saidia' ikitangaza Ligi Kuu haiwezi kusimamishwa

    (GMT+08:00) 2019-10-18 16:37:13
    Ligi Kuu ya soka ya Kenya (KPL) itaendelea jinsi ilivyopangwa, uongozi wa kampuni inayoendesha ligi hiyo KPL umesema na kuzionya klabukuwa ni lazima zifuate sheria zinazosimamia mchezo huo. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, KPL ilisema ilifikia uamuzi huo, licha ya wito wa kutaka ligi isimamishwe kutokana na ukosefu wa fedha wa ligi na klabu baada ya mdhamini wake mkuu SportPesa kujiondoa. Afisa Mkuu Mtendaji wa KPL, Jack Oguda amesema, ligi hiyo imejitolea kuendelea kuimarisha bidhaa yake, kutumia soka kuleta mema, kuunga mkono ukuaji wa soka na kufanya shughuli hiyo kwa uadilifu ili kulinda sifa na uimara wake. Afisa huyo amesema KPL imezungumza na kampuni kadha, lakini kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, ofa zilizowekwa mezani hazifikii mahitaji ya Ligi Kuu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako