• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ndayiragije atamba Stars kuiliza Sudan

  (GMT+08:00) 2019-10-18 16:47:24

  TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo itakuwa na shughuli pevu ugenini mbele ya Sudan katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN), utakaopigwa kwenye Uwanja wa Omdurman, mjini Khartoum. Kikosi hicho kinachonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije kitakuwa na mtihani mzito wa kushinda mchezo huo ili kunasa tiketi ya kwenda Cameroon. Akizungumzia mchezo huo, Ndayiragije alisema kikosi hicho kiko tayari kwa mapambano ya kusaka ushindi utakaowawezesha kuibwaga Sudan kwao na kutinga hatua ya makundi. Stars itashuka dimbani kuikabili Sudan ikiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo uliochezwa Septemba 22, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hiyo itahitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako