• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pato la taifa la China laongezeka kwa asilimia 6.2 katika robo tatu za mwanzo mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-10-18 18:56:02

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika robo tatu za mwanzo mwaka huu, pato la taifa la China GDP limezidi dola za kimarekani trilioni 9.87, na kuongezeka kwa asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.

  Msemaji wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Mao Shengyong ameeleza kuwa, katika kipindi hicho, uchumi wa China umeendelea kwa utulivu, ambapo muundo wake umeboreshwa, huku kiwango cha maisha ya watu kikiinuka kwa mfululizo, akisema,

  "Takwimu za awali zinaonesha kuwa, katika robo tatu zilizopita, pato la taifa la China limezidi dola trilioni 9.87 za kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki. Ongezeko katika robo hizo tatu ni asilimia 6.4, 6.2 na 6. Kwa kuangalia sekta tafauti, sekta ya kilimo imeongezeka kwa asilimia 2.9, sekta ya viwanda imeongezeka kwa asilimia 5.6, na sekta ya huduma imeongezeka kwa asilimia 7."

  Bw. Mao amesema, kasi ya ukuaji wa uchumi wa China imepungua kidogo, hata hivyo bado inashika nafasi ya mbele duniani. Akisema,

  "Kasi ya ongezeko la uchumi wa China katika robo tatu zilizopita ni asilimia 6.2, na imepungua kwa asilimia 0.1 kwa kulinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka huu. Inakadiriwa kuwa kasi hiyo bado ni kubwa zaidi kati ya nchi yenye ukubwa wa uchumi wa zaidi ya dola trilioni moja za kimarekani."

  Bw. Mao amesema, uchumi wa China unakabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini alama za hali ya uchumi ikiwa ni pamoja na ajira, mfumuko wa bei, na kipato cha raia bado ni nzuri. Hivi sasa mashirika mengi yanakadiria kuwa kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia huenda itaendelea kushuka. Akiulizwa kuhusu mwelekeo wa uchumi wa China katika robo ya nne ya mwaka huu, Bw. Mao amesema kuna mambo mengi chanya ya ndani, kwa mfano sekta ya huduma inaongezeka kwa kasi, matumizi yanaongezeka, sifa ya maendeleo ya uchumi inaongezeka, na ufanisi wa sera mpya unadhihirika, akisema,

  "Katika robo ya nne, tunaweza kuona mabadiliko na dalili nzuri, kwa mfano kasi ya ongezeko la sekta ya viwanda imeongezeka katika mwezi Septemba, uwekezaji wa miundombinu umefufuka katika miezi kadhaa iliyopita, na bei ya bidhaa za viwanda zimeongezeka. Nafikiri uchumi utaendelea kwa utulivu katika robo ya nne."

  Tangu mwaka 2006, China imeshika nafasi ya kwanza kwa kutoa mchango zaidi kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa miaka 13 mfululizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako