• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wasema Michezo ya 7 ya Majeshi Duniani itaongeza mawasiliano na kufunzana

    (GMT+08:00) 2019-10-20 17:49:51

    Maofisa na wataalamu kutoka nchi mbalimbali wamesema Michezo ya 7 ya Majeshi Duniani inayoendelea hapa China, ambayo ilifunguliwa rasmi Ijumaa jioni na rais wa China Xi Jinping huko Wuhan, mkoani Hubei, imetoa jukwaa la mawasiliano ya kirafiki na kufunzana miongoni mwa wanajeshi wa nchi mbalimbali.

    Viktor Baranets, mwandishi wa habari za kijeshi wa gazeti la Komsomolskaya Pravda la Russia, amesema michezo hiyo inaweza kuwaleta karibu wanajeshi, na kutoa mchango muhimu kwenye maendeleo na kuongeza kuelewana na kuwasiliana kati ya nchi tofauti. Naye mtaalamu wa mahusiano ya kimataifa wa Kenya anayeshughulikia uhusiano kati ya China na Afrika, Adhere Cavince pia amesema michezo hiyo inaonesha China haitaki kutumia nguvu za kijeshi kudhuri, kutishia au kulazimisha mataifa mengine kutekeleza matakwa yake katika medani ya kimataifa. Amesisitiza kuwa China inatumia fursa hii kuhimiza mbinu za kiuvumbuzi kwenye ushirikiano wa kijeshi, na kwamba maelewano na ushirikiano wa kijeshi ni vitu muhimu katika kulinda utulivu, usalama, amani na kujipatia maendeleo duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako