• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa sita wa mtandao wa internet duniani wafunguliwa China

    (GMT+08:00) 2019-10-20 17:50:51

    Mkutano wa sita wa mtandao wa internet duniani umefunguliwa leo mjini Wuzhen mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. Mkuu wa Idara ya uenezi ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Huang Kunming amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo, na kusoma barua ya pongezi kutoka kwa rais Xi Jinping wa China.   

    Kwenye barua hiyo, rais Xi amesema mwaka huu inatimia miaka 50 tangu kuzaliwa kwa mtandao wa internet. Kwa sasa, duru mpya ya mapinduzi ya teknolojia na mabadiliko ya sekta za uzalishaji yanaendelea kwa kasi, sekta ya mtandao wa internet inatiliwa nguvu mpya na nafasi nyingi zaidi za kimaendeleo. Na kwamba jumuiya ya kimataifa ina wajibu katika kuendeleza, kutumia na kusimamia vizuri mtandao wa internet, ili kuwanufaisha zaidi binadamu. Amebainisha kuwa nchi zote zinapaswa kufuata maendeleo ya zama mpya, kutekeleza wajibu wa maendeleo, kukabiliana na changamoto na kuhimiza kwa pamoja utatuzi wa migogoro duniani kwenye sekta hiyo, na kuhimiza kujenga jumuiya ya mtandao wa internet yenye mustakabali wa pamoja.

    Bw. Huang Kunming akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, amesema nchi zote duniani zinatakiwa kushikilia kunufaishana kwa usawa, kuaminiana kwa ushirikishi, kushikamana, kusaidiana, kuwasiliana na kufundishana, kuendeleza na kunufaika na uchumi wa kidigitali, kulinda usalama na utaratibu wa mtandao wa internet. Amesisitiza kuwa China ikiwa ni nchi kubwa yenye kuwajibika, itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kutoa mchango kwa maendeleo ya mtandao wa internet, kuhimiza ufunguaji mlango wa sekta hiyo, kulinda usalama na kusaidia kusimamia mtandao wa internet wa dunia, ili kuwanufaisha zaidi binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako