• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KIKAPU: Patriots yaishinda City Oilers na kuendeleza ubabe BAL Qualifiers

  (GMT+08:00) 2019-10-21 10:12:26

  Timu ya Rwanda Patriots imeingia raundi ya pili katika Ligi ya kufuzu Basketball ya Afrika (BAL) baada ya Jumamosi kuitoa kijasho chembamba timu ya Tanzania JKT na kuandikisha ushindi wao watatu mfululuzo kwenye kundi D. Mabingwa hao wa Rwanda jana waliungana na wenzao City Oilers ya Uganda ambapo timu hizo mbili zimefikia raundi ya pili na ya mwisho kwenye kundi lao D, zote mbili zikishinda michezo yao mitatu ya mwanzo. Katika mechi ya jana Patriots waliendeleza ubabe dhidi ya City Oilers kwa kupachika vikapu 74-63 mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Timu zote mbili zimeingia raundi ya pili ya Ligi ya kufuzu Basketball ya Afrika ambayo itachezwa kuanzia mwezi ujao hadi Disemba.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako