• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina mazingira mazuri, uwezo na imani katika kutimiza uchumi wake kupata maendeleo endelevu kwa hatua madhubuti

    (GMT+08:00) 2019-10-21 17:09:44

    Mkurugenzi wa Ofisi ya utafiti wa sera kwenye Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Yuan Da amesema, China ina mazingira mazuri, uwezo na imani katika kutimiza uchumi kupata maendeleo endelevu kwa hatua madhubuti.

    Takwimu kutoka Idara ya Takwimu ya China zimeonesha kuwa, katika robo tatu ya mwanzo ya mwaka huu, pato la ndani la nchi GDP liliongezeka kwa asilimia 6.2 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Bw. Yuan Da ameeleza kuwa, tokea mwaka huu, matatizo na changamoto mbalimbali zilizoikabili China zimeongezeka, na ni vigumu sana kwa uchumi wa China kuendelea kwa hatua madhubuti, muundo wa uchumi kuendelea kuboreshwa, huku maisha ya wananchi yakizidi kuboreshwa. Anasema:

    "Ongezeko la uchumi katika robo tatu zilizopita mwaka huu limepungua kwa kiasi, lakini sifa ya maendeleo inazidi kuinuka. Wakati uchumi wa China unapobadilika kutoka kupata maendeleo yenye kasi kubwa hadi maendeleo yenye sifa bora, kama kasi ya ongezeko la uchumi ikiwa juu au chini kidogo zote zinaweza kukubalika, ikiwa nafasi za ajira zitaongezeka, mapato ya wakazi yatainuka, mazingira ya ikolojia yataboreshwa na sifa ya maendeleo zitazidi kuongezeka hatua kwa hatua."

    Vilevile amesisitiza kuwa uchumi wa China bado unakabiliwa na shinikizo kubwa la kupungua. Anasema:

    "Tuna mazingira mazuri, uwezo na imani katika kutimiza uchumi kupata maendeleo endelevu kwa utulivu. Kwanza, sifa za mfumo wa kisiasa wa China, na ukubwa wa uchumi zimeifanya China iwe na uwezo mkubwa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuhakikisha utulivu wa uchumi. Pili, mazingira ya biashara yamezidi kuboreshwa. Tatu, msukumo wa maendeleo pia umezidi kuongezeka. Makampuni mengi yanafanya juhudi za kuimarisha utafiti na maendeleo ya teknolojia, kuhakikisha usalama wa mnyororo wa utoaji wa bidhaa, na kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ufanisi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako