• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China afanya ziara nchini Indonesia

    (GMT+08:00) 2019-10-21 17:18:08

    Makamu wa rais wa China Wang Qishan amemaliza ziara ya kirafiki nchini Indonesia kama mjumbe maalum wa rais Xi Jinping katika hafla ya kuapishwa kwa rais Joko Widodo wa Indonesia.

    Rais Widodo amesema, kitendo cha rais Xi kupeleka mjumbe maalum kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwake kunaonyesha uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili. Pia ameipongeza China kwa kutimiza miaka 70 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na kuitakia ustawi zaidi na kutoa mchango mkubwa zaidi katika amani na usalama wa dunia.

    Kwa upande wake, makamu wa rais wa China Wang Qishan amesema, China na Indonesia ni majirani wema, marafiki wazuri na wenzi wazuri, na kuongeza kuwa, uhusiano kati ya nchi hizo mbili una umuhimu mkubwa. Amesema China inathamini ahadi ya rais Widodo ya kuboresha uhusiano wa kimkakati wa pande mbili kati ya nchi hizo, na kuunganisha pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na mkakati wa maendeleo wa Indonesia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako