• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kuna kigezo kimoja tu dhidi ya vurugu

    (GMT+08:00) 2019-10-21 18:45:30

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema lazima kuwe na kigezo kimoja na msimamo mmoja dhidi ya vurugu, na kuongeza kuwa kitendo chochote chenye vigezo viwili kitajidhuru hatimaye.

    Amesema vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Cataluna nchini Hispania na zile za mjini London, Uingereza zinafanana na vurugu iliyotokea Hongkong, China. Lakini wanasiasa na vyombo vya habari kutoka nchi za magharibi wameona vurugu zilizotokea Hongkong, China ni kitendo cha "demokrasia na uhuru", na zimekuwa "vurugu" huko nchi za magharibi.

    Kutokana na kauli hizo, Bibi Hua Chunying amesema msimamo huo unaonyesha kuwa "demokrasia na haki ya binadamu" ni kisingizio cha nchi za magharibi katika kuingilia mambo ya Hongkong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako