• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani zinapaswa kuheshimiana na kutatua masuala kwa njia mwafaka

    (GMT+08:00) 2019-10-21 18:45:58

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, ushindani na tofauti kati ya China na Marekani zimekuwepo siku zote, jambo la muhimu zaidi ni kwamba pande zote mbili zinapaswa kuheshimiana na kutatua masuala kwa njia mwafaka.

    Alhamis iliyopita, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Bw. David Stilwell alisema uhusiano kati ya China na Marekani umeingia kwenye kipindi cha ushindani wa kimkakati, Marekani lazima ibadilishe njia yake ya kuitendea China, pia aliushutumu mfumo wa kijamii wa China bila ya msingi wowote.

    Akizungumzia kauli hiyo, Bibi Hua Chunying amesema kauli ya Stilwell inaonyesha maoni ya upande mmoja, fikra ya umwamba na vigezo viwili. Historia na hali halisi zinaonyesha kuwa sera ya ujamaa wenye umaalum wa China ni sahihi, na inalingana kabisa na hali ya China na mahitaji ya wananchi wa China, hivyo hakuna sababu ya kuibadilisha au kuiacha.

    Ameongeza kuwa China haitaathiriwa na wengine, itashikilia kithabiti njia yake sahihi, na Marekani inapaswa kuheshimu haki halali ya maendeleo ya nchi nyingine ikiwemo China kwa ushirikishi na usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako