• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa tatu wa ushirikiano wa maendeleo ya uchumi wa nchi za China na visiwa vya Pasifiki wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-10-21 19:13:36

    Mkutano wa tatu wa ushirikiano wa maendeleo ya uchumi wa nchi za China na visiwa wa Pasifiki umefunguliwa leo huko Apia, nchini Samoa. Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Hu Chunhua amehudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kusoma barua ya pongezi kutoka kwa Rais Xi Jinping wa China.

    Kwenye barua hiyo, rais Xi amesema mkutano huo ni makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi za visiwa vya Pasifiki, na anatumai kwamba pande hizo mbili zitatumia kikamilifu jukwaa hilo muhimu kuimarisha mazungumzo, kubadilishana uzoefu, kushirikiana na kukuza ushirikiano mkubwa kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Hu amesema, China ina nia ya kufanya kazi na pande zote kutekeleza makubaliano ya viongozi, kuimarisha uoanishaji wa kimkakati, kukuza ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kubadilishana uzoefu wa maendeleo. Pia kuboresha uwezo wa maendeleo, kupanua biashara na uwekezaji, na kukuza ushirikiano katika mambo ya kilimo, misitu, uvuvi, rasilimali ya nishati, bahari na utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako