• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

    (GMT+08:00) 2019-10-22 17:19:32

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jana amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi Ikulu mjini Paris, Ufaransa.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Macron amesema anatarajia kufanya tena ziara ya kiserikali nchini China na kuhudhuria Maonyesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa, pia kuinua kiwango cha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi mbili. Pia anataka kuhimiza ushirikiano kwenye sekta mbalimbali za uchumi na biashara, kilimo, fedha, nishati ya nyuklia kwa matumizi ya umma, na mawasiliano ya kijamii.

    Kwa upande wake, Wang Yi amesema kutokana na hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara zinazoikabili dunia kwa sasa, China na Ufaransa zinahitaji kushirikiana katika kulinda utaratibu wa dunia wenye pande nyingi, mamlaka ya Umoja wa Mataifa, na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa. Amesema China inaipongeza Ufaransa kwa juhudi zake kwenye sekta za kuhimiza umoja wa nchi za Ulaya, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuhifadhi anuwai ya viumbe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako