• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki za Afrika Masahriki zatajwa kuwa miongoni mwa bora duniani

    (GMT+08:00) 2019-10-22 19:19:16

    Jarida la kila mwezi la Uingereza The banker limezema benki za Afrika Mashariki ni miongoni mwa bora duniani.

    Jarida hilo limesema benko hizo ni miongoni mwa 1,000 bora na zenye kuhimili mazingira magumu ya soko na kiuchumi.

    Kulingana na jarida hilo benki kama vile KCB, Equity, Diamond Trust na Co-operative Bank, ziliandikisha ukuaji wa faida licha ya mazingira magumu.

    Kwa wastanbi benki duniani zilipata faida ya asilimia 2 ambayo ni sawa na dola trilioni 1.13 mwaka 2019 ikilinganishwa na trilioni 1.11 za mwaka 2018.

    Baadhi ya sababu za ukuaji wa polepole kulingana na jarida hilo ni mapja na mahitaji ya juu ya mtaji, ushindani kutoka kwa kampuni za teknolojia zinazohusu fedhana riba za chini hasa ulaya na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako