• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mihuri ya kielektroniki kuanza kutumika mwezi ujao.

  (GMT+08:00) 2019-10-22 19:19:36

  Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda URA imesema itaanza kutumia mihuri ya kielektroniki mwezi ujao.

  Hata hivyo chama cha watengenezaji bidhaa nchini humo kinaiomba serikali kuhahirisha mpango huo unaotarajiwa kuanz mwezi ujao.

  Maji, pombe na sigara ni baadhi ya bidhaa zitakazohitajika kuwa na muhuri huo.

  URA imesema bidhaa za aina hiyo zilizotengenezwa nani ya nchi au kuagizwa kutoka nje lazima zitumie muhuri wa kieletroniki.

  Mamlaka hiyo imesema mashine za mihuri hiyo zitawekwa katika majumba ya watengezaji bidhaa yaliosajiliwa.

  Watakaokaidi mpango huo mpya watatozwa ushuru mara mbili au kulipa faini ya shilingi milioni 50.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako