• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia yaomba kusamehewa madeni

  (GMT+08:00) 2019-10-22 19:19:55
  Waziri wa fedha wa Somalia Abdirahman Duale Beileh amesema nchi hiyo inapanga kuanzisha miradi ya kadhaa ya kupunguza umaskini ikiwa wakopeshaji wake wataisamehe madeni ya dola bilioni 5.

  Abdirahman amesema serikali imepiga hatua kwenye mazungumzo ya kusamehewa madeni na maafisa wa Marekani, Uingereza, benki ya dunia na shirika la fedha duniani IMF.

  Amesema Marekani imeonesha nia ya kuisamehe Somalia deni lake kwa kuzingatia utendaji wa kuridhisha wa Mogadishu kuelekea msamaha huo.

  Jumamosi IMF ilielezea kuunga mkono Somalia kusamehewa madeni hivi karibuni.

  Somalia inadaiwa dola bilioni 4.7 na IMF imesema kuwa nchi hiyo haiwezi kumudu kulipa au kuendelea kukopa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako