• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yakaribisha ATM za maziwa

  (GMT+08:00) 2019-10-22 19:20:44
  Kaimu Msajili wa Bodi za Maziwa Nchini, Sofia Mlote, ameeleza kufurahishwa na ujio wa teknolojia mpya ya ununuzi wa maziwa kwa njia ya mashine za ATM.

  Mlote alisema ujio wa mashine hizo utarahisisha wananchi wa Kilimanjaro kunywa kiwango sahihi cha maziwa ambacho ni lita 200 kwa mwaka kwa mtu.

  Alieleza imani yake hiyo wakati wa mahojiano na vyombo vya habari kuhusu teknolojia mpya mashine za ATM za maziwa ambazo zimewekwa katika wilaya za Hai na Manispaa ya Moshi.

  Alisema kwa sasa Mtanzania anakunywa lita 49 za maziwa kwa mwaka, wakati anatakiwa kunywa lita 200.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako