• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Njoroge atajwa kuwa Gavana Bora wa benki kuu

  (GMT+08:00) 2019-10-22 19:21:03
  Gavana wa Benki Kuu ya Kenya (CBK) Patrick Njoroge ametawazwa kama Gavana Bora wa benki katika mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakati wa tuzo ya mwaka huu ya watungaji sera bora, maarufu kama '2019 Global Markets Award'.

  Alipokea tuzo hiyo, jijini Washington D.C., Amerika.

  Hii ni mara ya pili kwa Dkt Njoroge kupata tuzo hiyo, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2016 wakati alituzwa kutokana na juhudi zake za kupambana na mfumkobei.

  Na katika tuzo yake ya mwaka 2019, ilitokana na uongozi wake wa kufanikisha shughuli ya kubadilishwa kwa noti za zamani za Sh1000 na noti mpya za thamani hiyo bila kuvuruga uthabiti katika soko la kifedha nchini, ilivyofanyika nchini India mnamo 2015.

  Shughuli hiyo iliendeshwa kati ya Juni 1 na Septemba 2019 kikiwa ni kipindi cha miezi mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako