• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la tatu la "Njia Hariri Baharini ya Karne ya 21" lafanyika

    (GMT+08:00) 2019-10-22 21:07:22

    Kongamano la tatu la mawasiliano ya kimataifa la China la "Njia Hariri Baharini ya Karne ya 21" limefanyika leo mjini Zhuhai mkaoni Guangdong, China.

    Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya "Ujenzi wa Eneo la kiuchumi la ghuba ya Guangdong, Hongkong na Macao kuhimiza kuunganisha 'Njia Hariri Baharini'" limeandaliwa na Shirika kuu la Utangazaji la China (CMG) pamoja na serikali ya Guangdong.

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano hilo, mkuu wa idara ya uenezi ya mkoa wa Guangdong Bw. Fu Hua amesema, mkoa huo ni kituo muhimu cha mawasiliano kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja", utaendelea kuimarisha mageuzi, kupanua ufunguaji mlango, kushirikiana na Hongkong na Macao katika kupanua masoko yaliyoko kwenye "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Mjumbe wa Idara ya uhariri kwenye Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) Bw. Hu Bangsheng amesema, Shirika hilo linaunga mkono kikamilifu ujenzi wa eneo la kiuchumi la ghuba ya Guangdong, Hongkong na Macao, kuanzisha makao makuu ya eneo hilo na kituo kikuu cha mkoa wa Guangdong mjini Guangzhou, pia kuanzisha kituo cha eneo hilo mjini Shenzhen, na kushirikiana na mkoa wa Guangdong kwenye sekta za kutengeneza tamthilia, teknolojia mpya ya 5G, na 4K/8K. Amesema CMG inapenda kushirikiana na vyombo vya habari vya nchi mbalimbali katika kuboresha mazingira ya utangazaji wa kimataifa, kuimarisha ushirikiano wa vipindi, kuhimiza maendeleo ya mafungamano ya vyombo vya habari, ili kuistawisha Njia Hariri kwa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako