• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  LANGALANGA: Mercedes ina wasiwasi wa kushinda Mexican Grand Prix  wikiendi hii

    (GMT+08:00) 2019-10-23 09:04:12

    Mercedes imesema wanatazamia kuwa na wakati mgumu katika mbio za Mexican Grand Prix wikiendi hii ambapo Lewis Hamilton anatapa kulitia mkononi taji la mashindano hayo. Hamilton atakuwa amenyaka ubingwa mara sita duniani kama atamzidi dereva mwenzake wa Mercedes Valtteri Bottas angalau kwa pointi 14. Hata hivyo hicho kinaonekana ni kibarua kigumu sana kwani Mercedes haifikirii kwamba barabara za Mexico City zinafaa kwa gari zao. Bosi wa timu ya Mercedes Toto Wolff amesema mbio nne zilizosalia hazitakuwa rahisi lakini za Mexico ndio zitakuwa ngumu zaidi, kwani barabara zilizo uwanda wa juu zitawapa changamoto kubwa ambapo upepo wenye ujazo mdogo unasababisha gari isitulie barabarani na hata kuleta matatizo ya utendaji wa injini. Mercedes imepata taji laola sita mfululizo katika mbio za Japan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako