• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari wa Marekani walioondoka Syria hawakupata ruhusa ya kukaa Iraq

    (GMT+08:00) 2019-10-23 09:05:46

    Jeshi la Iraq limesema askari elfu 1 wa Marekani walioondoka kaskazini mashariki mwa Syria walipata ruhusa ya kupita Iraq tu, na hawakupata ruhusa ya kukaa nchini humo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamandi ya operesheni ya pamoja ya Iraq, askari hao ambao hawakuwa na ruhusa ya kukaa, watahamishwa kutoka Iraq. Mapema kabla ya hapo waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper amesema askari elfu moja wa Marekani walioondolewa kaskazini mashariki mwa Syria, wamepelekwa magharibi mwa Iraq kupambana na kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako