• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Manchester City yaipiga Atalanta 5-1

    (GMT+08:00) 2019-10-24 17:27:54
    Stiker Raheem Sterling alifunga mabao matatu kwa mara ya kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya na kuisaidia klabu yake ya Manchester City kuibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Atalanta ya Italia katika pambano la Kundi C. Sergio Aguero aliongeza mabao mawili. Atalanta ilifunga penalti kupitia kwa Ruslan Malinovskyi baada ya Fernandinho kumuangusha Josip Ilicic. Sterling ambaye ndiye mfungaji wa mabao mengi ya City baada ya kuifungia klabu hiyo ya EPL mara 12 katika mechi 13 za mashindano tofauti, msimu huu alisema kuna mengine mazuri njiani. Kocha wake, Pep Guardiola alimsifu kama mchezaji aliyeimarika zaidi kutokana na nguvu zake za ziada awapo uwanjani. Kwenye mechi hiyo, Rodri aliondolewa baada ya kuumia, huku Phil Foden akionyeshwa kadi nyekundu, hii ikiwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako