• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na shirika lisilo la kiserikali zatoa wito wa kutoingilia kati mambo ya ndani ya China

    (GMT+08:00) 2019-10-24 17:37:46

    Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Ushauri wa Kisheria ya Asia na Afrika (AALCO) zimetoa wito wa kutoingilia kati mambo ya ndani ya China, ikiwa ni kutokana na hali iliyoko sasa kaika mkoa wa Hong Kong, China.

    Wito huo ulitolewa Jumanne usiku katika hafla ya kusherehekea Mpango wa Utafiti na Mawasiliano wa China na AALCO ulioingia mwaka wake wa tano. Waziri wa Katiba na Masuala ya Sheria nchini Tanzania Dr. Augustine Mahiga aliwaambia watu waliohudhuria hafla hiyo kuwa, suala la Hong Kong ni suala la ndani la China.

    Akisisitiza kuwa Hong Kong ni sehemu ya China, Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke amesema, China haitaruhusu nguvu za nje kuingilia masuala ya Hong Kong, pia haitaruhusu mapinduzi ya aina yoyote kuchukua nafasi katika mkoa huo. Amesema serikali ya China inaunga mkono kikamilifu serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong kuchukua hatua zozote za lazima kuendana na sheria kutoa adhabu kwa vitendo vya uhalifu wa kimabavu, kudumisha utawala wa sheria, na kurejesha utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako