• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya Wafanyabiashara ,Wakulima,na Wenye Viwanda Vidogo Zanzibar wahimizwa kuingia soko la EAC

  (GMT+08:00) 2019-10-24 19:47:53
  Waziri wa Biashara,Balozi Amina Salum Ali,ameishauri Jumuiya ya Wafanyabiashara ,Wakulima,na Wenye Viwanda Vidogo Zanzibar,kutumia fursa wanazozipata kuingia katika ushindani wa kibiashara kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

  Katika kikao na Jumuiya ya Wafanyabiashara,Wakulima na Wenye Viwanda Vidogo,ofisini kwake Migombani jana,Waziri huyo alisema serikali iko tayari kushirikiana na wafanyabiashara kuimarisha mikakati ya kibiashara kwa wafanyabiashara wakubwa,wa kati,na hata wadogo.

  Alisema Wizara ya Biashara na Viwanda itafanya juhudi zote kushirikiana katika mpango wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na zenye kiwango ili kusaidia kuwaongeza nguvu ya kuyatumia masoko ya Afrika Mashariki.

  Aidha alitaka jumuiya hiyo kuyatumia masoko hayo ikiwamo pia kufikisha bidhaa na huduma zao Congo,Sudan na Msumbiji ili kukuza kiwango cha kibiashara hadi ikifika Julai mwakani,Zanzibar iwe imaeshaonyesha matunda ya biashara hiyo.

  Naye Mwenyekiti wa JUmuiya ya Wafanyabiashara,Wakulina na Wenye Viwanda Vidogo,Toufiq Turky alisema gharama kubwa zinzotozwa kwenye mizigo ambazo zinafikia zaidi ya mara tatu zinachangia katika kurudisha nyuma maendeleo ya kibiashara.

  Alisema iwapo matatizo ya usafirishaji wa bidhaa yatafanyiwa marekebisho itasaidia kukuza kiwango cha biashara na kitafikia ushindani wanaoulenga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako