• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na tishio la usalama

  (GMT+08:00) 2019-10-24 20:37:42

  Rais Vladimir Putin wa Russia huko Sochi amesema, nchi yake itazisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto kubwa na tishio la usalama, ikiwemo ugaidi.

  Rais Putin amesema hayo katika hafla ya kuwakaribisha viongizi wa nchi za nje wanaoshiriki kwenye mkutano wa kwanza wa wakuu kati ya Russia na Afrika. Amesema, nchi hiyo itaunga mkono nchi za Afrika kutekeleza sera ya uhuru na kujitegemea, kufanya juhudi kushirikiana na nchi za Afrika kutatua migogoro, kuzuia ugaidi na msimamo mkali, kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka na magendo ya dawa za kulevya. Pia amesema, Russia inapenda kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na nchi za Afrika juu ya msingi wa usawa, urafiki na kuheshimiana.

  Ameeleza imani yake kuwa, vikao mbalimbali vitakavyofanyika na mafanikio yatakayopatikana katika mkutano huo utazidi kuongeza mawasiliano kati ya Russia na nchi za Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako