• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuandaa michuano ya kwanza ya Kombe la Dunia la Klabu lililoongezwa timu 24

  (GMT+08:00) 2019-10-25 08:38:44

  Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Gianni Infantino jana alitangaza kuwa China itaandaa michuano ya kwanza ya Kombe la Dunia la Klabu lililoongezwa timu 24 na kusifu kuwa ni uamuzi wa kihistoria. Akitoa tangazo hilo baada ya mkutano wa Baraza la Fifa huko Shanghai, Infantino amesema mashindano yatafanyika Juni na Julai mwaka 2021. Hakutoa ufafanuzi zaidi lakini amesema mashindano yatakuwa na timu nane kutoka Ulaya, moja kutoka China, moja kutoka Oceania na tatu kutoka mashirikisho ya bara jingine. Infantino amethibitisha kuwa China, ambayo imefanya soka kuwa kipaumbele cha taifa chini ya rais Xi Jinping, imekuwa mgombea pekee. Amesema vigezo vya kuchagua timu vitaamuliwa katika wiki chache zijazo, lakini Atletico Madrid, Real Madrid, Chelsea na Liverpool watashiriki kwa vile hizo ni timu nne washindi wa makombe ya Ulaya. Kombe la Dunia la Klabu kwa sasa lina timu saba na linafanyika kila Disemba. Qatar itaandaa michuano miwili ya mwisho, ukiwemo wa mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako