• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yatoa chanjo ya polio na surua, na rubella kwa zaidi ya watoto milioni 18.7

  (GMT+08:00) 2019-10-25 08:54:40

  Wizara ya Afya nchini Uganda imesema imetoa chanjo ya polio, surua, na rubella kwa zaidi ya watoto milioni 18.7 walio na umri wa chini ya miaka 15.

  Waziri wa wizara hiyo Ruth Aceng amewaambia wanahabari kuwa, zaidi ya watoto milioni 18.7 wamepata chanjo, ikiwa ni zaidi ya lengo la watoto milioni 18.1 lililowekwa. Amesema watoto milioni 7.3 walio na umri wa chini ya miezi minane walipewa chanjo dhidi ya polio.

  Kampeni hiyo ya kitaifa ya siku tano ilianza jumatano wiki iliyopita lakini iliongezwa siku moja kutokana na mahitaji makubwa ili kukabiliana na kuenea kwa magonjwa ya surua na rubella ambayo yameathiri sehemu kadhaa nchini Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako