• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNESCO yaunga mkono mpango wa Zambia wa kukabiliana na ndoa za utotoni

    (GMT+08:00) 2019-10-25 08:59:28

    Nchi wanachama wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) jana zimekubaliana kuunga mkono mpango wa Zambia kuhusu kukabiliana na ndoa za utotoni na mimba za utotoni na zisizotarajiwa.

    Mwakilishi wa kudumu wa UNESCO nchini Zambia Bi. Christine Kseba-Sata amewashukuru wanachama wa shirika hilo kwa kuunga mkono mpango huo.

    Kseba-Sata amesema, ndoa na mimba za utotoni zinaongezeka kwa kasi, haswa katika nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara na za kusini mwa Asia, ambapo viwango vya hali hiyo vinaweza kufikia asilimia 38, na viwango vya mimba za utotoni barani Afrika vimefikia asilimia 15 hadi 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako