• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa watoa wito wa uwekezaji kwa ajili ya ukarabati baada ya Kimbunga Idai

  (GMT+08:00) 2019-10-25 09:00:12

  Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (ECA) jana imesema, zaidi ya dola za kimarekani bilioni 4 zinahitajika kusaidia ukarabati katika nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe kutokana na athari mbaya ya Kimbunga Idai ambacho kilizikumba nchi hizo tatu mapema mwaka huu.

  Kutokana na taarifa iliyotolewa na kamati hiyo, Msumbiji iliyokumbwa na kimbunga Idai na Kenneth, inahitaji dola za kimarekani bilioni 3.2 kwa ajili ya juhudi za ukarabati wake, Malawi inahitaji dola za kimarekani milioni 370 na Zimbabwe inahitaji dola za kimarekani miliooni 600 hadi 700.

  Wajumbe kutoka nchi hizo tatu wamesisitiza kuwa, nchi hizo zimeshindwa kupata msaada wa kutosha wa kifedha ili kujenga upya maisha na kufanya ukarabati haraka baada ya kimbunga Idai na Kenneth.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako