• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa kilele kati ya Russia na Afrika wafungwa

    (GMT+08:00) 2019-10-25 09:39:20

    Mkutano wa kwanza wa kilele kati ya Russia na nchi za Afrika umefungwa mjini Sochi, Russia, baada ya kupitisha taarifa ya pamoja inayoweka wazi malengo na majukumu ya pande hizo mbili katika kukuza ushirikiano wa sekta mbalimbali. Kufuatia taarifa hiyo, Russia na nchi za Afrika zimeamua kususia kwa pamoja vikwazo vya kisiasa na kifedha katika ushirikiano wa biashara ya kimataifa, na kutumia vigezo tofauti katika uhusiano wa kimataifa. Aidha, Russia na nchi za Afrika zitashirikiana katika mapambano dhidi ya ugaidi. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 40 za Afrika na wajumbe wa nchi 11 na mashirika ya kiafrika na ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako