• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Polisi wa Somalia wakabidhi watuhumiwa wawili wa kigaidi wa Al-Shabab kwa Kenya

  (GMT+08:00) 2019-10-25 14:34:59

  Polisi wa Somalia wamewakabidhi watuhumiwa wawili wa ugaidi wa kundi la Al-Shabab kwa polisi wa Kenya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuzuia mashambulizi ya kuvuka mipaka.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kaskazini mashariki nchini Kenya Paul Soi amesema, watu hao wawili wanaaminika kukimbilia Somalia baada ya kufanya uhalifu katika kanda hiyo na hasa karibu na mpaka wa Liboi.

  Polisi wamesema, wapiganaji hao wanahusika na shambulizi lililotokea tarehe 12 Oktoba huko Liboi, ambapo polisi 11 waliuawa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako