• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka za kodi katika nchi za Afrika zajitahidi kupunguza mianya ya kupotea kwa kodi

  (GMT+08:00) 2019-10-25 19:11:11

  Mamlaka za kodi za nchi za Afrika zitaadhimisha miaka 10 ya baraza la mamlaka za kodi Afrika ATAF katika juhudi zao za kupunguza mianya ya kodi.

  Jumla ya nchi 38 ni wanachama wa baraza hilo, na kulifanya baraza hilo kuwa ni chombo kikubwa zaidi duniani kinachohusika na mambo ya kodi.

  Mwakilishi wa Uganda kwenye baraza hilo Bibi Stella Nyapendi, amesema baraza hilo limekuwa likitoa huduma za ushauri kuhusu mambo ya kodi, na limezisaidia nchi wanachama kujenga uwezo kwa wajumbe wake kupunguza kuvuja kwa kodi. Pia amesema baraza hilo linashirikiana na taasisi kama Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA, jopo la ngazi ya juu kuhusu usafirishaji haramu wa fedha (IFF) na mtandao wa haki kuhusu kodi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako