• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China kufanya ziara nchini Uzbekistan na Thailand

    (GMT+08:00) 2019-10-25 19:24:55

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atafanya ziara nchini Uzbekistan na Thailand kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi ujao, na anatarajia kuhudhuria mkutano wa 18 wa Baraza la viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO mjini Tashkent nchini Uzbekistan, na kuhudhuria mkutano wa 22 wa viongozi kati ya China na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini na Mashariki ASEAN, mkutano wa 22 wa viongozi kati ya China, Korea Kusini, Japan na ASEAN, na mkutano wa 14 wa wakuu wa nchi za Asia Mashariki mjini Bangkok nchini Thailand.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema kwenye mikutano hiyo Bw. Li Keqiang atabadilishana maoni na viongozi kuhusu kuhimiza maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikano ya Shanghai, na kuimarisha kuunganisha kwa pamoja ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", pendekezo la ushirikiano wa kikanda na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali, na kuhimiza ushirikiano kwenye sekta za biashara, uwekezaji wa uwezo wa uzalishaji, mawasiliano na jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako