• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wasiorejeshe mikopo ya Benki Tanzania taabani

  (GMT+08:00) 2019-10-25 21:01:22
  Benki kuu ya Tanzania (BoT) imezindua kanzi data, itakayowezesha upatikanaji wa taarifa za fedha za wakopaji ili kuwatambua wafanyibiashara wanaokopa na kushindwa kurejesha fedha kwa wakati. Benki hiyo itafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Dun and Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited.

  Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa fedha katika benki kuu ya Tanzania bwana Jerry Sabi, amesema mfumo huo utaziwezesha taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wingi.

  Tayari BoT imetoa leseni kwa kampuni hiyo ili ianze kuandaa taarifa za wakopaji kutoka kwenye kanzidata ya Benki Kuu.Aidha, mfumo huo utasaidia benki na taasisi zinazotoa mikopo kuwatambua wakopaji wasumbufu na kupunguza mikopo chechefu.

  Mfumo huo pia utaongeza uwajibikaji katika kukopesha na kukopa, pia kusaidia wakopeshaji na wadai, kusimamia vitabu vyao vya mkopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako