• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Peter Ndegwa ndiye afisa mkuu mtendaji wa Safaricom

  (GMT+08:00) 2019-10-25 21:01:44
  Peter Ndegwa ametangazwa Afisa Mkuu Mtendaji mpya wa kampuni ya Safaricom; nafasi ambayo imekuwa ikishikiliwa na Michael Joseph kama kaimu tangu kufariki kwa Bob Collymore Julai 1, 2019. Hatua hii inajiri siku moja tu baada ya Joseph kuwaambia wanahabari hiyo juzi kwamba uamuzi ulikuwa haujaafikiwa.

  Ndegwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni kubwa ya bia ya Diageo; hasa operesheni za Uropa na Urusi kuanzia Julai 2018 kufikia sasa. Ataanza kazi rasmi Safaricom kuanzia Aprili 2020.

  Awali aliwahi kuwa afisa mkuu wa kampuni ya Guinness Nigeria Breweries Plc, ambayo ni tawi la Diageo.

  Aidha, Ndegwa alijiunga na kampuni ya East African Breweries Limited mnamo Januari 2004 na akawa hapo kama Mkurugenzi wa Fedha na alikuwa amewahi kufanya kazi katika PricewaterhouseCoopers.

  Kati ya mwaka 2011 na 2015, alikuwa Meneja Mkurugenzi wa Guinness Ghana Breweries.

  Awali duru zilikuwa zimesema kwamba Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Safaricom ilikuwa imekosa kukubaliana kuhusu uteuzi wa afisa mkuu mpya kuchukua nafasi ya Boby Collymore aliyefariki miezi mitatu iliyopita.

  Duru zilikuwa zimesema kuwa wanachama wa bodi hiyo waliokutana Jumanne usiku walikuwa wamekosa kuafikiana kuhusu suala hilo.

  Bw Joseph aliteuliwa kushikilia wadhifa wa huo kwa muda kutoa nafasi ya kuteuliwa kwa mtu atakayejaza nafasi rasmi.

  Kwa muda mrefu, kumekuwepo na madai kwamba mshikilizi wa cheo hicho ulicheleweshwa kutokana na mivutano ya kimasilahi katika kampuni hiyo huku ikidaiwa kuwa serikali ilitaka kuwa na usemi mkubwa ikizingatiwa kuwa ina asilimia 35 ya hisa katika kampuni hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako