• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • URA yanasana lita 800 za Mafuta feki ya injini

    (GMT+08:00) 2019-10-25 21:02:04

    Maafisa wa polisi kutoka wilya ya Mbale wamewatioa mbaroni wanawake watatu ambao wanadaiwa kuwauzia madera na waendeshaji pikipiki Mafuta ghushi ya injini. Watatu hawa walitiwa nguvuni kufuatia msako mkali uliofanywa na mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda, URA ka ushirikiano na maafisa wa polisi. Akithibitisha kukamatwa kwa watatu hawa, msemaji wa polisi eneo la Elgon, bwana Robert Tukei, alisema kwamba lita 800 za mafuta ghushi ya injini zilipatikana.

    URA imekuwa mstari wa mbele kukabiliana na wafanyibiashara walaghai. Ni hivi juzi tu ambapo URA ilifunga baadhi ya biashara jijini Kampala kwa kile kilichotajwa kuwa ukwepaji wa kulipa ushuru. Mwaka wa 2007, shirika la kuthibiti ubora wa wa bidhaa nchini Uganda lilinasa makatoni 50 ya mafuta aina ya Gatex ambayo hayakuwa yenye ubora stahiki, katika eneo la Mbale.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako