• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda ni taifa la pili Afrika kwa urahisi wa kufanya biashara

  (GMT+08:00) 2019-10-25 21:02:23
  Rwanda ni taifa la pili barani Afrika lenye mazingira mazuri ya kufanyia biashara. Hii ni kulingana na ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia hivi juzi kuhusiana na jinsi ya kufanya biashara afrika. Kulingana na ripori hiyo kwa jina Doing Business 2020, Rwanda ni moja ya mataifa barani Afrika ambayo yamezidi kujiimarisha katika maswala ya uchumi na biashara kwa mwaka ulioisha Mei mosi mwaka huu. Taifa linaloongoza Afrika kwa urahisi wa kuendesha biashara ni Mauritius.

  Duniani, Rwanda ni nambari 38 kutoka 29 mwaka uliopita, huku ikiwa na pointi 76.3 kwa 100. Rwanda inajivunia kuwa na miundo msingi thabiti, urahisi wa kupata nguvu za umeme na urahisi wa kupata leseni za kufanya biashara hali kadhalika ujenzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako