• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China apongeza mkutano wa kilele wa wanasayansi vijana duniani

  (GMT+08:00) 2019-10-26 18:11:31

  Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa mkutano wa kilele wa wanasayansi vijana duniani uliofunguliwa leo mjini Wenzhou, mkoani Zhejiang, China.

  Rais Xi amesema, hivi sasa mageuzi ya teknolojia na sekta za sayansi yanapamba moto, na mustakabali wa sayansi na teknolojia unategemea vijana. Amewahimiza wajumbe wa mkutano huo kubadilishana maoni, kufunzana, kuimarisha msingi wa urafiki, na kuongeza ushirikiano, ili kuanzisha mustakabali mzuri zaidi wa bindamu.

  Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na karibu wajumbe 800 wakiwemo wanasayansi waliopewa tuzo ya Nobel, wanataaluma, wanasayansi vijana maarufu na viongozi wa mashirika ya kimataifa ya sayansi na teknolojia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako