Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema takriban watu laki 9.8 wakiwemo wakimbizi wa ndani, wakimbizi, na jamii za wenyeji wamepoteza makazi yao au kuathirika na mafuriko kutokana na msimu wa mvua kubwa sehemu za kaskazini mwa Sudan Kusini.
OCHA imebainisha kuwa mafuriko kwenye kaunti 32 za Jonglei, Upper Nile, Equatorial ya Mashariki, Bahr el Ghazal ya Kaskazini, Unity na mikoa ya Lakes yamekuwa makubwa zaidi na kuwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula katika nchi hiyo changa. Kwa mujibu wa taarifa, zaidi ya silimia 60 ya kaunti zilizoathiriwa na mafuriko sasa zimewekwa kwenye ngazi ya maeneo yanayokabiliwa na utapiamlo mkubwa unaotokana na mafuriko tangu mwezi Julai.
Wakati huohuo Umoja wa Mataifa na washirika wake wanatafuta karibu dola milioni 90 za Kimarekani ili kutoa msaada wa haraka wa kibinadamu na uungaji mkono wa kuwapatia nafuu wahanga milioni 2.3 wanaokabiliwa na msimu wa ukosefu wa mvua kusini mwa Zambia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |