• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Magufuli wa Tanzania akutana na ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China

  (GMT+08:00) 2019-10-27 15:34:48

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania CCM ambaye pia ni rais wa nchi hiyo Bw. John Magufuli amekutana na ujumbe wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC unaoongozwa na naibu mkuu wa idara ya mawasiliano ya kamati kuu ya chama hicho Bw. Guo Yezhou kwenye ikulu ya Dar es Salaam.

  Rais Magufuli amemshukuru Rais Xi Jinping wa China kwa kumpa waziri mkuu wa zamani wa Tanzania Bw. Salim Ahmed Salim Medali ya Urafiki, na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kueneza kwa nguvu urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili na kukuza maendeleo ya uhusiano kati ya vyama hivyo viwili na nchi hizo mbili.

  Naye Bw. Guo Yezhou amesema kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kiko tayari kuendeleza mbele urafiki wa jadi na CCM, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, na kuhimiza uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye kiwango kipya.

  Wakati wa ziara hiyo, rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na katibu mkuu wa CCM Bw. Bashiru Ali, na wajumbe wengine pia wamekutana na ujumbe huo kwa nyakati tofauti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako