• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idadi ya watu waliokufa kufuatia mvua kubwa nchini Tanzania yafikia 40

  (GMT+08:00) 2019-10-27 18:18:33

  Polisi nchini Tanzania wamesema idadi wa watu waliokufa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo imeongezeka kutoka 30 hadi kufikia 40.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Inspekta Edward Bukombe amesema gari lililokuwa linasafirisha watu 10 lilisombwa na maji jana, wakati dereva akijaribu kupitisha gari hilo kwenye daraja la mto uliofurika wilayani Handeni na kufanya idadi ya jumla ya watu waliokufa kufikia 40. Kamanda Bukombe amesema dereva alitahadharishwa kupitisha gari kwenye daraja hilo kwa kuwa limevunjika, lakini hukusikia.

  Alhamisi Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania ilitoa tahadhari ya tatu ndani ya mwezi huu, ikisema mvua zitaendelea kunyesha kwa siku tano mfululizo kuanzia Alhamisi. Katika mikoa ya Tanga, Kagera na Geita, na katika visiwa vya Unguja na Pemba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako