• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • GDP ya Tanzania yaongezeka kwa asilimia 7.2 katika robo ya pili mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-10-28 08:50:21

  Ofisi ya Takwimu nchini Tanzania NBS imesema uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 7.2 katika robo ya pili ya mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 6.1 ya mwaka jana kipindi kama hicho.

  Ripoti iliyotolewa jana na ofisi hiyo inasema, kukua kwa kasi kwa Pato la Ndani la Taifa GDP kati ya Aprili na Juni mwaka huu kunatokana na kuboreshwa kwa utendaji wa sekta za ujenzi, madini na mawasiliano.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika kipindi hicho, sekta ya ujenzi ilirekodi ukuaji wa kasi zaidi wa asilimia 19.6, ikifuatwa na asilimia 17.2 kwenye sekta ya madini na asilimia 10.3 katika sekta ya habari na mawasiliano.

  Ripoti pia inasema serikali ya Tanzania inatarajia kuwa ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu mzima utafikia asilimia 7.1, ikilinganishwa asilimia 7 ya mwaka jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako