• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa mataifa wasema utaiunga mkono serikali ya mpito nchini Sudan

  (GMT+08:00) 2019-10-28 08:54:44

  Umoja wa mataifa umeeleza kuwa utaiunga mkono serikali ya mpito ya Sudan kufikia demokrasia, kufufua uchumi na amani.

  Kwenye sherehe ya siku ya Umoja wa mataifa iliyosherehekewa jana mjini Khartoum, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Bibi Amina Mohamed amesema Umoja wa mataifa utamuunga mkono Waziri mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok na serikali yake, kwa serikali yake inatoa kipaumbele kwa uongozi wa wanawake na ushiriki wao, na kushirikisha vijana kwenye mipango ya maendeleo.

  Waziri mdogo wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Siddiq Abdul-Aziz amesema serikali ya Sudan itafuata misingi ya utawala bora na utawala wa sheria, na kuiweka nchi kwenye njia ya mageuzi ya kisiasa na kufufua uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako